Mapya yaibuka katika sakata la tuhuma dhidi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kilwa Hanan Mohamed Bafagih, anaedaiwa kuhusika na kipigo cha kijana aliyeishia kupoteza nguvu za kiume

habarimedia Avatar
Get more from Evarist Chahali in the Substack app
Available for iOS and Android

Jana, kijarida hiki kilichapisha tuhuma dhidi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Hanan Mohamed Bafagih, adaiwa kuhusika na kipigo cha kijana aliyeishia kupoteza nguvu za kiume.

Kama hukubahatika kusoma habari hiyo, bonyeza hapa chini

Kijarida hiki kimetumiwa ujumbe kutoka kwa watu wawili tofauti wanaofahamu kuhusu suala hili

Kiongozi habari, hide my id, hiyo issue ya dogo kilwa ni kweli ilitokea na hizo fedha ni kweli Mkurugenzi alisema kapoteza.

Lakini ataarifa za chini ya kapeti ni kwamba fedha zilikua ni za ziara ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu. Hata hivyo, zilibaki na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wakagawana.

Hao madogo wameteswa sana bila kosa. Vilevile, Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa na TAKUKURU wanajua, lakini hata kumhoji Mkurugenzi hizo shilingi milioni 17 kazitoa wapi walishindwa.

Pia taarifa ilipelekwa TAKUKURU Kilwa ila wao walikaaa kimya, waliogopa kumhoji huyo Mkurugenzi kwa sababu ana undugu na Rais Samia. Na ni kweli wamemhanisi huyo kijana kutokana na kipigo na mateso which is not fair at all.

Mdau mwingine alieleza kwamba mtumishi wa Manispaa ya Kilwa alirejea taarifa ya awali iliyoeleza

Tarehe 18/09/2023 Nyumbani Kwa Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Kilwa Aitwaye Hanan D/O Mohamed Bafagih, 29 Yrs. Mzanzibar Muislamu Mkazi Wa Kilwa Masoko Kuliripotiwa Tukio La Wizi (Jalada Klm/Ir/523/2023 Lahusika).

3. Mkurugenzi Huyo Alikuwa Anaishi Nyumba Na Chumba Kimoja Na Rafiki Yake Wa Kike Aitwaye Fatuma D/O Ayubu Mandari, 36yrs. Mchaga, Muislamu, Psychologist Mkazi Wa Masoko Ambaye Ndiye Anayetunza Funguo Za Nyumba Na Funguo Za Chumba.

4. Katika Tukio Hilo Ziliibwa Fedha Taslim Sh.14,000,000/= Na Mikufu Miwili Ya Dhahabu Yenye Thamani Ya Sh. 10,000,000/= Hivyo Kufanya Thamani Ya Jumla Sh 24,000,000/=.

Mdau huyo alieleza kwamba katika mazingira ya kawaida tu, Mkurugenzi huyo wa kike kuishi chumba kimoja na mwanamke mwezie, ambaye baadaye alikuja kuwa mmoja wa watuhumiwa, ilipaswa kuzua maswali.

Mdau huyo amedai kuwa ni siri ya wazi katika Manispaa hiyo kuhusu “mahusiano yasiyo ya kimaadili anayojihusisha nayo Mkurugenzi huyo”.

Kijarida hiki kilielezwa bayana aina ya mahusiano hayo lakini kinahifadhi kwa sababu za kimaadili.

MENGINEYO

Tagged in :

habarimedia Avatar

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *